Mchungaji Prudence Chuwa ambaye alikuwa akihudumu katika Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront kwa kipindi cha miaka takribani kumi, amehamishiwa katika usharika jirani wa Mbezi Beach ulioko hapa jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati wa kuwaaga washarika wa Azaniafront, Mchungaji Chuwa aliwashukuru washarika kwa kumpa ushirikiano wa kutosha kwa kipindi chote ambacho alihudumu usharikani hapo. "Baada ya kuhudumu kwa miaka kumi hapa, nimepata nafasi ya kufahamiana na watu wengi na ninashukuru sana kwa ushirikiano ambao mmenipatia kwa sababu umeniwezesha kutimiza majukumu yangu vizuri", alisema Mchungaji Chuwa.

Habari kwa kina itaendelea .........................