WAKRISTO wametakiwa kujua kwamba uchaguzi ni sehemu ya maisha ya kila siku, hivyo wanapochagua hawana budi kuangalia yale yanayompendeza Mungu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Pili wa Jimbo la Kilimanjaro Kati, Mch. Israeli Moshi wakati alipokuwa akihubiri Neno la Mungu katika Ibada maalum ya harambee ya kuchangia ununuzi wa eneo la ujenzi wa Kanisa iliyofanyika Usharika wa Longuo, Mtaa wa Kifumbu mkoani Kilimanjaro. Mch. Moshi alisema kuwa hata kwenye imani kumekuwa na watumishi wa aina nyingi kwa hiyo ni kazi ya Mkristo kuchagua yupi ni wa kweli na yupi siyo wa kweli.

Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi wa Usharika huo, Richard Njau aliwataka Wakristo kujitoa katika kutoa kwani kuna baraka pale wanapotoa kwa moyo na kuwataka kuotoa ili kazi iliyopo mbele yao ya ujenzi wa Kanisa iweze kukamilika.

"Hata kwenye imani kumekuwa na watumishi wa aina nyingi kwa hiyo ni kazi ya Mkristo kuchagua yupi ni wa kweli na yupi siyo wa kweli."