WANAFUNZI 591 wa shule ambazo ziko chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), wamepata ufaulu wa daraja la kwanza katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa wiki iliyopita, sawa na asilimia 21.4 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani katika shule hizo za KKKT. WANAFUNZI hao ni sehemu ya watahiniwa 522,217, sawa na asilimia 97.66 ya watahaniwa wote waliofanya mtihani huo.

Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Athumani Amasi alisema jumla ya watahiniwa kutoka shule 456,975 kati ya 520,558 walifanya mtihani huo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Diakonia, KKKT, Dk. Paul Mmbando, KKKT ina jumla ya shule za sekondari 67, lakini shule zilizofanya mtihani huo ni 59.

Hii ni kutokana na kwamba baadhi ya shule za Kanisa hilo bado hazifikia kidato cha nne, kutokana na kuanzishwa hivi karibuni. Uchunguzi uliofanywa na Upendo umebaini kwamba wanafunzi waliofanya mtihani kupitia shule hizo za KKKT ni 2,776 lakini kati yao saba matokeo yao yamezuiliwa, hivyo yaliyopo ni ya wanafunzi 2,769.

Uchambuzi wa UPENDO unaonyesha kuwa wanafunzi 956 sawa na asilimia 34.5 walipata daraja la pili, huku wanafunzi 746 sawa na asilimia 27 wakiwa wamepata daraja la tatu. Kwa upande wa daraja la nne limebeba wanafunzi 460 sawa na asilimia 16.6. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa ni wanafunzi 15 tu, sawa na asilimia 0.5 ndiyo waliopatadaraja sifuri.

Kwa matokeo hayo, jumla ya wanafunzi 2754 sawa na asilimia 99.4 wa shule hizo za KKKT, wamefaulu mtihani huo uliofanyika mwaka jana.

Akizungumzia matokeo ya shule za Kanisa kwa ujumla, Mkurugenzi wa Elimu, KKKT, Christowaja Mtinda alisema wanajivunia kuona shule za Kanisa zikiendelea kufanya vizuri ikilinganishwa na miaka mingine. Alisema hiyo imetokana na mikakati madhubuti inayofanywa na Kanisa katika kuboresha sekta ya elimu.

Mojawapo ya mikakati ambayo ilipangwa kwa baadhi ya shule katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani ilikuwa ni kuondoa daraja sifuri na daraja la nne. Alisema pamoja na mikakati ya Kanisa kupitia Dayosisi zake na mtalaa mpya uliotolewa na Serikali, lakini siri iliyofanya zifanye vizuri ni namna maadili na nidhamu vinavyosimamiwa na kuzingatiwa Katika matokeo hayo ya shule za KKKT, shule ya Seminari Ndogo ya Agape ya Dayosisi ya Kaskazini, imeongoza kwa kuwa na wanafunzi 91 waliopata daraja la kwanza, 29 wa daraja la pili na daraja la tatu ni wanafunzi 5.

Hakuna daraja la nne wala sifuri. Mkuu wa Seminari hiyo, Mchg. Godrick Lyimo, alisema kinachowabeba wanafunzi hao ni kuishi kwa malezi ya Kikristo, pamoja na kuwa na maombi ya asubuhi mchana na jioni. Mchg. Lyimo aliongeza kwamba, pia wanawafundisha kufanya kila jambo kwa wakati sahihi na kuwahimiza kusoma kwa bidii.

WALICHOSEMA WAKUU WA SHULE

Mkuu wa Shule ya Sekondari Image, iliyopo Dayosisi ya Iringa, Joshua Lyandala, alisema shule yao imefanya vizuri hivyo wanapaswa kujipongeza, kwani hawana sifuri na wana mikakati ya kuendelea kuongeza mbinu za ufundishaji ikiwemo muda wa ziada wa kufundisha ili wazidi kufanya vizuri. Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Hope Lutheran, ya Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mchg. Jonathan Kyaruzi, aliwaomba wazazi kuwa na imani na shule za Kanisa kwani zinafanya vizuri na wanafundisha maadili mema.

Mwl. Kyaruzi alisema wanafundisha wanafunzi kuwa na hofu ya Mungu na kuwafundisha jinsi ya kuishi na watu kwa unyenyekevu, kwani wanategemewa hapo baadaye kuzisaidia familia zao na Taifa. Halikadhalika Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Hull Kijota, iliyopo Dayosisi ya Kati, Thomas Yusuph, alisema ushirikiano mzuri baina ya wazazi na walimu unachangia shule hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mtihani na kuwaomba wazidi kuiamini.

Mwl. Yusuph alibainisha kwamba, shule yao huwa inamfundisha mtoto malezi bora ya kuwaheshimu watu wengine, kuwa na utii na kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa kazi mbalimbali wanazowapa wanafunzi, ili wawaelekeze kwa undani zaidi.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Usa-River Rehabilition ya Dayosisi ya Meru, Emanuel Ayo alifafanua kuwa shule hiyo inahudumia watu wenye ulemavu wa viungo na kuiomba jamii iwapeleke watoto hao katika shule hiyo kwani wana miundombinu rafiki. Mwl. Ayo alisema shule hiyo pamoja na kwamba ni mara ya kwanza kuwa na watahiniwa wa kidato cha nne, walijitahidi kuwapa maswali ya mara kwa mara ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mtihani wao.

DAYOSISI YA KASKAZINI (MOSHI)

Shule ya Bishop Moshi Sekondari, wanafunzi waliopata daraja la kwanza walikuwa 3, daraja la pili 5, daraja la tatu 1 na daraja la nne 12 hawana daraja sifuri. Shule ya Sekondari Kidia hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza, daraja la pili imepata wanafunzi 3, daraja la tatu 7, daraja la nne 4, lakini hakuna daraja sifuri.

Katika shule ya Nronga Sekondari wanafunzi waliopata daraja la kwanza 4, daraja la pili 4, daraja la tatu 6, daraja la nne 16 hakuna mwanafunzi aliyepata daraja sifuri. Nayo shule ya wasichana ya Masama daraja la kwanza 19, daraja la pili 43, daraja la tatu 11, daraja la nne 4 hawana daraja sifuri.

Kwa upande wa Msufini Sekondari imepata wanafunzi wa daraja la kwanza 6, daraja la pili wanafunzi 6, daraja la tatu wanafunzi 15, daraja la nne wanafunzi 10, shule hii haikuwa na mwanafunzi aliyepata daraja sifuri. Shule ya Natiro Sekondari, shule hii imepata daraja la kwanza 5, daraja la pili 27, daraja la tatu 13, daraja la nne 14 na daraja sifuri mwanafunzi 1. Kwa shule ya Vunjo Sekondari wanafunzi 4 wamepata daraja la kwanza, daraja la pili, 12, daraja la tatu 13, daraja la nne 6 hawana daraja sifuri.

Shule ya Sekondari Uroki, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza, daraja la pili ni wanafunzi 5 pekee, daraja la tatu 8, daraja la nne 8 hakuna mwanafunzi wa daraja sifuri. Shule ya Sekondari Boloti daraja la kwanza 4, daraja la pili 9, daraja la tatu 4 hakuna daraja la nne wala daraja sifuri.

Shule ya Mtakuja Sekondari daraja la kwanza 11, daraja la pili 20, daraja la tatu 10, daraja la nne 2 hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri. Kwa upande wa shule ya Sekondari ya Sisters of Ushirika wa Neema daraja la kwanza wanafunzi 11, daraja la pili 14, daraja la tatu 14, daraja lanne 9 hakuna sifuri.

DAYOSISI YA KASKAZINI MAGHARIBI (BUKOBA)

Shule ya Sekondari Iluhya daraja la kwanza 16, daraja la pili 36, daraja la tatu 31, daraja la nne 4 na hakuna sifuri. Bukoba Lutheran Sekondari hii shule daraja la kwanza wako 21, daraja la pili 28, daraja la tatu 18, daraja la nne 3 na hakuna sifuri. Bukoba Hope Lutheran Sekondari daraja la kwanza wako wanafunzi 48, daraja la pili 32, daraja la tatu 7, daraja la nne 2 na hakuna aliyepata sifuri katika shule hiyo.

DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI (LUSHOTOTANGA)

Shule ya Sekondari Lwandai daraja la kwanza ni wanafunzi 3, daraja la pili 6, daraja la tatu 11, daraja la nne 3 na hakuna sifuri. Seminari ndogo ya Kilutheri Bangala hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza, daraja la pili ni wanafunzi 2, daraja la tatu 3, daraja la nne 2 na hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri.

DAYOSISI YA KUSINI (NJOMBE)

Shule ya Sekondari Kidugala imepata wanafuzi 40 wa daraja la kwanza, darala la pili 32, daraja la tatu 7 daraja la nne na hakuna aliyepata sifuri. Shule ya Wasichana Emmaberg daraja la kwanza wako 6, daraja la pili 10, daraja la tatu 27, daraja la nne 13 na hakuna aliyepata daraja sifuri. Shule ya Wasichana Igumbilo Lutheran Sekondari daraja la kwanza 38, daraja la pili 50, daraja la tatu 11 na hakuna waliopata daraja la nne wala sifuri.

Shule ya Wasichana Mufindi Lutheran Sekondari ina wanafunzi 22 waliopata daraja la kwanza, daraja la pili ni wanafunzi 34, daraja la tatu wanafunzi 19 na daraja sifuri hakuna mwanafunzi aliyelipata.

DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI (DAR ES SALAAM)

Kisarawe Lutheran Junior Seminary, daraja la kwanza ina wanafunzi 12, daraja la pili wanafunzi 15, daraja la tatu 9, daraja la nne 6 hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri. Shule ya Sekondari Mbwawa, daraja la kwanza ni wanafunzi 6, daraja la pili 8, daraja la tatu 3 hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la nne wala sifuri. Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkuza ina wanafunzi 4 waliopata daraja la kwanza, daraja la pili 16, daraja la tatu wanafunzi 10, daraja la nne 9 hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri.

DAYOSISI YA KATI (SINGIDA)

Dayosisi hii ina shule ya Sekondari Iambi ambayo ina wanafunzi 3 waliopata daraja la kwanza, daraja la pili 7, daraja la tatu 13, daraja la nne 9 na mmoja alipata sifuri. Sekondari ya Hull Kijota daraja la kwanza ni wanafunzi 5, daraja la pili 13, daraja la tatu 10, daraja la nne 6 na hakuna aliyepata daraja sifuri. Shule ya Sekondari Ihanja, ina mwanafunzi 1 aliyepata daraja la kwanza, daraja la pili 5, daraja la tatu 7, daraja la nne 7 hakuna daraja sifuri katika shule hii.

DAYOSISI YA MBULU

Shule ya Sekondari Dongobesh ina wanafunzi wa daraja la kwanza 11, daraja la pili 36, daraja la tatu 21, daraja la nne 14 na mmoja amepata sifuri. DAYOSISI YA PARE Shule ya Sekondari Dindimo daraja la kwanza ni sifuri, daraja la pili sifuri, daraja la tatu wawili na daraja la nne 6 hakuna mwanafunzi aliyepata daraja sifuri. Shule ya Sekondari Manka hawana daraja la kwanza wala la pili, daraja la tatu 2, daraja la nne 7 na daraja sifuri 4.

DAYOSISI YA KARAGWE

Shule ya Sekondari Karagwe daraja la kwanza 16, daraja la pili 25, daraja la tatu 19, daraja la nne 7 hakuna aliyepata sifuri. Kwa upande wa shule ya Sekondari Benard daraja la kwanza ni wanafunzi 2, daraja la pili 13, daraja la tatu 22, daraja la nne 11 na hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri.

Shule ya Sekondari ya Wasichana Bweranyange, waliopata daraja la kwanza ni wanafunzi 3, daraja la pili 12, daraja la tatu wanafunzi 12, daraja la nne mwanafunzi mmoja na hakuna aliyepata sifuri. D

AYOSISI YA KUSINI KATI (MAKETE)

Shule ya Sekondari Bulongwa, mwanafunzi mmoja ndiye aliyepata daraja kwanza 1, daraja la pili 7, daraja la tatu 7, daraja la nne 14 hakuna aliyepata sifuri.

DAYOSISI YA KONDE (TUKUYU-MBEYA)

Seminari ndogo ya Kilutheri Manowa, aliyepata daraja la kwanza ni mmoja, daraja la pili 7, daraja la tatu 3, daraja la nne 4 na hakuna aliyepata sifuri.

DAYOSISI YA KASKAZINI KATI (ARUSHA)

Shule ya Sekondari Enaboishu; daraja la kwanza 4, daraja la pili 14, daraja la tatu 22, daraja la nne 15 na hakuna aliyepata sifuri. Shule ya Sekondari Peace House daraja la kwanza 12, daraja la pili 31, daraja la tatu 34, daraja la nne 7 na mmoja alipata sifuri. Kwa upande wa shule ya Sekondari Moringe Sokoine, daraja la kwanza 4, daraja la pili 18, daraja la tatu 24, daraja la nne 6, hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri.

Shule ya Sekondari ya Wasichana Maasae, daraja la kwanza wanafunzi 6, daraja la pili 36, daraja la tatu wanafunzi 23, daraja la nne 2 hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri. Katika shule ya Sekondari Ngateu hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza, daraja la pili 2, daraja la tatu 6, daraja la nne 19 na mmoja alipata sifuri. Shule ya Sekondari Kimandolu wanafunzi waliopata daraja la kwanza 20, daraja la pili 8 na hakuna walipata madaraja ya tatu, nne wala sifuri.

DAYOSISI YA IRINGA

Shule ya Sekondari Image, daraja la kwanza ni wanafunzi 19, daraja la pili 22, daraja la tatu 26, daraja la nne 14 hakuna aliyepata sifuri. Shule ya Sekondari Pomerini waliopata daraja la kwanza ni 8, daraja la pili 18, daraja la tatu 23, daraja la nne 9 na hakuna aliyepata sifuri. Shule ya Sekondari Mtera daraja la kwanza 1, daraja la pili 10, daraja la tatu 19, daraja la nne 22 hawana daraja sifuri. Kwa shule ya Sekondari Bomalang’ombe daraja la kwanza 4, daraja la pili 5, daraja la tatu 7, daraja la nne 15 na hakuna aliyepata sifuri.

Shule ya Sekondari Ipalamwa hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza, daraja la pili 3, daraja la tatu 2, daraja la nne 13 na wawili walipata sifuri. Shule ya Sekondari Lutangilo; aliyepata daraja la kwanza ni mmoja, daraja la pili wanafunzi 20, daraja la tatu wako 18, daraja la nne 16 na hakuna aliyepata sifuri.

DAYOSISI YA DODOMA

Aya Shule ya Sekondari daraja la kwanza ni wanafunzi 7, daraja la pili 15, daraja la tatu 14, daraja la nne 5 na hakuna aliyepata sifuri. Shule ya Sekondari Embeko daraja la kwanza wanafunzi 2, daraja la pili wanafunzi 14, daraja la tatu wanafunzi 11, daraja la nne wanafunzi 8 hakuna daraja sifuri katika shule hii.

DAYOSISI YA MKOANI MARA

Shule ya Sekondari Samaritan Technical School, waliopata daraja la kwanza ni 13, daraja la pili 16, Daraja la tatu 10, daraja la nne 1 na hakuna aliyepata sifuri. DAYOSISI YA MERU Ailanga Lutheran Junior Seminary Wanafunzi waliopata daraja la kwanza katika shule hii ni 23, daraja la pili 33, daraja la tatu 10, daraja la nne 1 na hawana mwanafunzi aliyepata sifuri. Shule ya Sekondari Makumira, wanafunzi 8 wamepata daraja la kwanza, daraja la pili ni wanafunzi 16, daraja la tatu wanafunzi 19, daraja la nne 13 na mmoja alipata sifuri.

Shule ya Sekondari Kikatiti daraja la kwanza 3, daraja la pili 16, daraja la tatu 30, daraja la nne 32 na hkuna aliyepata sifuri. Kwa upande wa Shule ya Sekondari Ngarenanyuki wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni 13, daraja la pili 23, daraja la tatu 19, daraja la nne 7 na hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri.
Shule ya Sekondari Usa River Rehabilition, wanafunzi 6 wamepata daraja la kwanza, daraja la pili 2, daraja la tatu 4, daraja la nne wanafunzi 9 na hakuna aliyepata sifuri.

DAYOSISI YA KUSINI MAGHARIBI (MATAMBA)

Shule ya Sekondari Itamba, waliopata daraja la kwanza ni wanafunzi 5, daraja la pili wanafunzi 6, daraja la tatu 6, daraja la nne wanafunzi 11 na waliopata sifuri ni wanafunzi 3. Dayosisi ya Ulanga Kilombero Seminari ya Kilutheri Tumaini (Shule ya Sekondari) aliyepata daraja la kwanza ni mmoja, daraja la pili ni mwanafunzi 1, daraja la tatu 4, daraja la nne 4 hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri.

DAYOSISI YA KUSINI MASHARIKI ZIWA VICTORIA (SHINYANGA/SIMIYU)

Shule ya Sekondari Mwadui, daraja la kwanza wanafunzi 15, daraja la pili wanafunzi 58, daraja la tatu 28, daraja la nne wanafunzi 12 na hakuna aliyepata sifuri.

DAYOSISI YA MWANGA

Shule ya Wasichana ya Sekondari Usangi, hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la kwanza wala daraja la pili, daraja la tatu ni wanafunzi 3, daraja la nne wanafunzi 6 hakuna mwanafunzi aliyepata sifuri.