ASKOFU wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk. Msafiri Mbilu amewataka Wakristo kuwa na desturi ya kuandaa sadaka wanazozipeleka madhabahuni, ili Mungu aweze kuzitakabali na kuruhusu baraka zake kwenye maisha yao.

Askofu Mbilu ameyasema hayo wakati akiongoza Ibada ya sikukuu ya mavuno, Jimbo la Pwani, Usharika wa Kana hivi Jumapili Akihubiri neno la Mungu kwenye Ibada hiyo kutoka kitabu cha Mwanzo 4:2b-7, Askofu Dk. Mbilu aliwakumbusha waumini wa Dayosisi hiyo. 2

Awali akitoa salamu za Ofisi Kuu ya Dayosisi kwa Washarika wa Kana, Askofu Dk. Mbilu aliwakumbusha wana KKKT-DKMs umuhimu wa kumtumikia Mungu kupitia matoleo, hasa akikazia mfuko wa maendeleo ambao unaviwezesha vituo mbalimbali vya Dayosisi kuihudumia jamii.

Askofu Dk. Mbilu pia aliendelea kuwakumbusha Wakristo kujiepusha na mafundisho potofu ambayo yanashika kasi katika nyakati hizi