Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex Malasusa amewasihi Wachungaji, Wainjilisti na Watumishi wengine katika Kanisa hilo kuacha kujihesabia haki katika utumishi wao badala yake waendelee kuwa wanyenyekevu mbele za Mungu.

Amesema hayo wakati akihubiri katika Ibada maalumu ya Watumishi wa Dayosisi hiyo ambayo imefanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front. 

Askofu Malasusa amewakumbusha watumishi hao kuwa wanalo jukumu la kuwafuata watu waliojitenga na Kanisa kwa kuanguka katika dhambi badala ya kuwaacha kwani mtu anapokuwa nje ya Utawala wa Mungu ni sawasawa na mtu aliyekufa.

Amesema kusudi la Mungu katika maisha ya watu ni kutaka wabadilike lakini siku hizi kumekuwa na ongezeko la huduma za Makanisa ambazo bado hazitimizi kusudio hilo badala yake zimekuwa kama sehemu za burudani tu.

Amesisitiza kuwa ukuaji wa Usharika au Mtaa kigezo cha kuangalia isiwe Sadaka na michango mingine bali iwe ni watu kumpokea na kumjua Mungu pamoja na Washarika kupokea Sakramenti