HATIMAYE zama za uongozi wa awamu ya tano Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Konde zimeanza rasmi baada ya Askofu Geoffrey Samwel Mwakihaba kuingizwa kazini rasmi na kusimikwa Jumapili iliyopita. ASKOFU Mwakihaba alisimikwa katika Ibada iliyofanyika Kanisa Kuu, Tukuyu katika Ibada iliyongozwa na Mkuu wa Kanisa, Askofu Dk Fredrick Shoo.

Tendo la kuingizwa kazini likiongozwa na Askofu Mstaafu wa Dayosisi hiyo Dk. IsraelPeter Mwakyolile, akishirikiana na Maaskofu Dk. George Fihavango wa Dayosisi ya Kusini na Amon Kinyunyu wa Dayosisi ya Dodoma. Kuanzia muda wa asubuhi hadi jioni ya Saa 10 mji wa Tukuyu uligubikwa na shangwe wakati Ibada hiyo ilivuta idadi kubwa ya watu ilipokuwa ikiendelea. Sh an gw e hi zo zili on g ozw a n a m a t a rumb e t a n a n yimbo w a k a ti maandamano ya kuanza Ibada hiyo yalipoanza Ofisi Kuu ya Dayosisi hiyo hadi viwanja vya Kanisa Kuu.

Polisi walisindikiza maandamano hayo na kuhakikisha usalama unakuwepo muda wote wa Ibada hiyo ya kihistoria. Askofu Mwakihaba anakuwa Askofu wa tano wa Dayosisi hiyo inayounda Dayosisi 26 za KKKT. Alitanguliwa na Maaskofu William Elijahu Mwakagali (1982 – 1990), Amon Dick Mwakisunga (1990- 2001), Dk. Israel Peter Mwakyolile (2001 2018) na Dk. Edward Mwaikali (2018 – 2022).

Kadhalika Askofu Mwakihaba aliingizwa kazini rasmi siku ambayo Dayosisi ya Konde ilikuwa ikitimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake. Dayosisi ya Konde ilizaliwa Juni 5, 1982 kutoka Dayosisi ya Kusini katika tukio ambalo lilipewa sura ya matengenezo baada ya mgogoro wa muda mrefu.

Mgogoro huo ulisababishwa na uamuzi wa aliyekuwa Askofu wa dayosisi hiyo, Mch. Dk Mwaikali kuamua kuhamisha makao makuu ya dayosisi kutoka Tukuyu kwenda Usharika wa Ruanda, jijini Mbeya. Hitimisho la mgomgoro huo lilikuwa ni uamuzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa Dayosisi ya Konde ambao ulipiga kura ya kutokuwa na Imani na Askofu Dk. Mwaikali na baadaye kumchagua Mch. Mwakihaba kuwa Askofu na Mch.Dk Meshark Njinga kuwa msaidizi wake.

IBADA YA WAKFU WA ASKOFU

Ibada ya kumwingiza kazini Askofu Mwakihaba, ilitanguliwa na tukio la kumwondolea wak fu wa Uasko fu, mtangulizi wake ambaye ni Mch. Dk. Mwaikali. Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Konde, Wakili Benjamin Mbembela alisoma hati iliyotokana na kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi ya Konde, ikieleza yatokanayo na uamuzi wa Mkutano Mkuu Maalumu wa dayosisi hiyo uliokaa Machi 22, 2022, katika Usharika wa Uyole jijini Mbeya.

Katibu Mkuu huyo alisema kuwa, Halmashauri Kuu ya Konde ilijadili vitendo vilivyofanywa na aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, Dk Mwaikali na kuomba Askofu Mwakyolile aondoe wakfu wa vifaa vya kiaskofu na kumwondolea wakfu wa Uaskofu na kutamka kuwa yeye siyo Askofu kwa mujibu wa taratibu za KKKT.

Baada ya kusomwa kwa hatia hiyo, Askofu Dk. Mwakyolile alisema kuwa Mkutano Mkuu maalumu uliokaa Machi 22, 2022 ulijadili utumishi wa Mwaikali na kuona kuwa amepoteza sifa za kuwa Askofu na Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Konde na kupiga kura ya kutokuwa na imani naye na kutakiwa arudishe vifaa vya kiaskofu. Askofu Mwakyolile alifanya maombi ya kutengua Uaskofu wa Mwaikali alioupata Januari 18, 2018.

Katika maombi yake Askofu Dk. Mwakyolile alinukuu mstari unaosema kuwa yoyote mtakayofunga duniani yatafungwa mbinguni na yoyote mtakayoyafungua dunia yatafunguliwa mbinguni. Katika maombi yake madhabahuni, Askofu Dk Mwakyolile alisema: “Badala ya Dayosisi kufanya kazi yake ya kiutume viongozi wake wamekuwa wakishinda mahakamani, wakilishtaki Kanisa lako kwa sababu hizo Dayosisi imepoteza kondoo wengi maana ushuhuda wa Kikristo umekosekana kabisa. Tunakusihi Mungu wetu linusuru Kanisa, inusuru Dayosisi, tufinyange kwa upya, ushuhuda wa Dayosisi upate kurudi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

“Nasogea mbele zako kwa moyo wa unyenyekevu nikikuomba, utengue sasa wakfu na mbaraka aliopewa, Mch. Edward Mwaikali, alipowekewa mikono na wazee 18.1 2018, alipofanyika kuwa Askofu wa kuchunga na kulisha kundi lako, Bwana Mungu ninakuomba utengue sasa, Mungu ninakuomba utengue Bwana Mungu ninakuomba utengue sasa, Amen.” Yalikuwa maombi ambayo yalifanya baadhi ya Washarika kububujikwa machozi.

Baada ya kumaliza kuomba, Askofu Mwakyolile ambaye Januari 18, 2028 ndiye aliongoza Ibada ya kumwingiza kazini Dk. Mwaikali, huku akiwa ameketi kwenye kiti akiwa ameshika fimbo ya Kichungaji na kusema: “Kwa mamlaka nliyopewa na Kanisa, kwa mamlaka niliyopewa na Mungu kwa njia ya Kanisa lake, mimi Askofu Israel Peter Mwakyolile, niliyemweka wakfu Mch Dk. Edward Mwaikali kuwa Askofu, natamka leo siku ya Bwana ya tano ya mwezi wa Juni 2022, mbele za Mungu anayetuona na mbele za umati wa watakatifu waliokusanyika hapa leo kushuhudia yanayofanyika kuwa, Mch Edward Jonson Mwaikali, siyo Askofu tena wa KKKT, Dayosisi ya Konde na Kanisa lote pia, katika jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, Amen.

VIFAA VYA UASKOFU NA KANISA KUU

Siku moja kabla ya kumwingiza kazini Askofu Mwakihaba, ilfanyika Ibada kuondoa wakfu jengo la Ibada la Usharika wa Ruanda, ambalo lilitangazwa kuwa Kanisa Kuu badala ya Kanisa Kuu la Tukuyu.

Askofu Mwakyolile aliondoa wakfu na kusema kuwa haiwezekani Dayosisi moja kuwa na Makanisa Makuu mawili na baada ya hapo aliongoza Ibada ya kuondoa wakfu vifaa vya Kiuaskofu vilivyokuwa vikitumiwa na Dk. Mwaikali. Katika Ibada hiyo ya utangulizi iliyofanyika Jumamosi ya Juni 4, 2022 Askofu Dk. Mwakyolile aliwaeleza Washarika kuwa walimshauri Dk. Mwaikali avirejeshe vifaa hivyo ili vitumiwe na Askofu mwingine lakini alikataa.

“Tunatakiwa tutengue vifaa hivyo kwa sababu Mkutano Mkuu ulitengua Uaskofu wa Edward Mwaikali na hata baada ya kumshauri alikatalia vifaa hivyo,” alisema Askofu Dk. Mwakyolile. Wakati hayo yakifanyika Kanisa lilikuwa kimya.

Askofu Dk. Mwakyolile aliviondolea wakfu vifaa hivyo ambavyo ni kiti cha Kiuaskofu, fimbo ya kichungaji, pete, msalaba na mavazi ya Kiuaskofu aliyokuwa akiyatumia Dk. Mwaikali. Katika sehemu ya maombi yake Askofu Dk. Mwakyolile huku akiwa amepiga magoti madhabahuni alisema: “

Mkutano Mkuu umetengua Uaskofu wa Mwaikali na kumtaka arejeshe na vifaa vinavyotumika katika Kanisa lako, vifaa hivyo hadi leo havijarejeshwa, tunakuja mbele zako tukikuomba utengue wakfu uliowekwa kwenye vifaa vile na ubariki vifaa tutavyoviweka wakfu leo. Kisha akasimama na kugeukia Washarika na kusema:

“Kwa mamlaka niliyopewa na mamlaka ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania natamka kwamba, vifaa vilivyotumika katika Dayosisi ya Konde yaani fimbo ya kichungaji, pete pamoja na msalaba na kiti cha uaskofu na mavazi yake, leo wakfu huo umetanguliwa rasmi katika jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu Amen.”

Baada ya kuomba hivyo alianza Ibada ya kuviweka wakfu vifaa vipya kwa ajili ya kutumiwa na Askofu Mwakihaba. Kabla Ibada hiyo iliyofanyika mchana, kulikuwa na shamrashama za aina yake kwani wakati Mkuu wa KKKT anawasili vigelegele vilisikika na hali hiyo iliendelea hata pale alipowasili aliyekuwa Askofu Mteule, Mwakihaba