MKUTANO Mkuu (Sinodi) wa 15 wa Uchaguzi wa Dayosisi ya Kati (Singida), umemchagua Mchg. Dkt. Sypirian Hilinti kuwa Askofu Mteule wa Dayosisi hiyo baada ya kupigiwa kura za ndiyo 424 kati ya kura 427. Mchg.

Hilinti ni Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo inayoongozwa na Askofu Dk. Alex Mkumbo ambaye anamaliza muda wake baada ya kuongoza tangu tangu Januari 6, 2013.

Mkutano huo ambao umefanyika Juni 22 hadi Juni 24 mwaka huu, Usharika wa Makao Makuu ya Uaskofu -Imanueli ulipo mjini Singida, pia umemchagua Mchg. Dkt. Zephania Shilla, kuwa Msaidizi wa Askofu Mteule kwa kupata kura za ndiyo 426 kati ya kura zote zilizopigwa ambazo ni sawa na asilimia 100.

Askofu Mteule Hilinti atakuwa Askofu wa tano wa Dayosisi hiyo akiwa ametanguliwa na Maaskofu Dk. Amos Gimbi, (1987-1999), Gidion Mghina (1999-2005), Eliufoo Sima (2006- 2012) na Dk. Alex Mkumbo (2013-2022).