Ibada za mitandaoni zapata umaarufu

TEXAS, MAREKANI

PAMOJA na mabadiliko ya haraka ya hali na miongozo mipya juu ya COVID-19 kuhusiana na mikusanyiko mikubwa, Makanisa mengi yamegeukia kuwa na Ibada za mtandaoni na kufanikiwa kuhudhuriwa na mamilioni ya watu.

Ushuhuda wa mafanikio hayo ulitolewa na Mchungaji Joel Osteen ambaye alifuta huduma zake zote za Ibada katika Kanisa la Lakewood huko Houston, Texas zilizokuwa zikifanyika kila mwishoni mwa wiki ili ambapo baada ya kuchukua hatua hiyo mahubiri ya Osteen yalirushwa katika mitandao kama Facebook, YouTube, Roku, AppleTV kwenye tovuti yake,JoelOsteen.com.

"Tuliona watu milioni nne na nusu wakifuatilia Ibada yetu kwa njia ya mtandao jumapili iliyopita mwishoni mwa wiki kwenye majukwaa yote, hii ilivunja rekodi yetu ya awali ya milioni 4.17 mnamo Novemba mwaka jana wakati Kanisa liliposhirikiana katika huduma ya Jumapili na mwanamuzki  Kanye West na naamini Idadi hii inaweza kuongezeka kwa kila wiki  ”alisema Mchungaji Osteen.

Katika toleo lililopita la Gazeti hili kulikuwa na habari juu ya watu zaidi ya laki moja kumpokea Yesu kwa kupitia Mkutano wa Injili uliyofanyika mtandaoni na kuhudhuriwa na mamilioni ya watu kutoka maeneo mbalimbali duniani, hiyo inaonesha kuwa kwasasa watu wengi wanahudhuria Ibada za mitandaoni kuliko mahudhurio ya Ibada za kawaida zilizokuwa  zikifanyika Kanisani.

Kwa mujibu wa Christian Post, inaonesha kuwa kipindi hiki cha ugonjwa wa corona watu wengi wamekuwa wakiwa na uhitaji wa kuwa karibu zaidi na Mungu ili kupata faraja na matumaini katika wakati huu mgumu kwa dunia nzima.

Mwanzoni mwa mwezi machi kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, kilipendekeza kwamba kusiwe na makusanyiko ya watu ili kuzua  kuenea kwa virusi kwa wingi.

Kituo hicho cha kudhibiti na kuzuia magonjwa kilisema kuwa "Hafla kubwa na mikusanyiko kubwa inachangia kuenea kwa COVID-19 nchini Marekani mfano wa hafla kubwa na mikusanyiko ya watu ni pamoja na mikutano, sherehe na Ibada”.

Makanisa kote marekani yameendelea kusambaza huduma zao mitandaoni hadi pale hali itakapokuwa imekaa sawa utafiti uliofanywa na taasisi ya LifeWay ya huko Nashville ulionyesha kuwa sio kila Kanisa ambalo linaweza kufanya huduma mtandaoni.

This news is from UPENDO, the weekly newspaper of ELCT Estern and Coastal Diocese.
Follow us on Facebook , Instagram and Youtube.