Katibu Mkuu wa Umoja wa Kiinjili wa Kimisioni (UEM) Afrika Mchungaji, Dkt. VOLKER MARTIN amewasili nchini ambapo anatarajia kutembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa kwa ushirikiano na Dayosisi mbalimbali nchini.

Akizungumza baada ya kuwasili amesema kuwa anayofuraha kubwa kwa mara nyingine kufika katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani kwa ajili ya kujionea Maendeleo mbalimbali yaliyofikiwa baada ya kipindi kirefu kupita kutokana na changamoto za COVID-19.

Naibu Katibu Mkuu wa UEM, Mchungaji ERNEST KADIVA amesema ziara ya Katibu Mkuu imelenga kuimalisha zaidi ushirikiano baina yao na huku akisema wanatarajia kujifunza zaidi namna ya kukabiliana na changamoto ambazo zinajitokeza

Kaimu Katibu Mkuu Dayosisi Mchungaji WILBROAD MATSAI amesema kama Kanisa wanayofuraha kutembelewa na katibu mkuu huyo na wanatarajia kufaidika zaidi na ziara yake hasa katika Mipango ya Maendeleo

Dayosisi nyingine zitakazotembelewa na Katibu huyo ni Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dayosisi ya Kaskazini Mgharibi, Dayosisi ya Karagwe, atakutana na Mkuu wa KKKT Dkt. FREDRICK SHOO,n pia atatembelea chuo cha Tumaini Makumila.