HISTORIA

USHARIKA huo ulianzishwa Machi 9, 2003 ukiwa na Washarika 30 na hii ilitokea baada ya wakazi Walutheri wa eneo hilo kutambuana na kisha kufikiri namna ya kushiriki Ibada ya pamoja ambaye baadaye aliamua kumtoea Bwana sehemu ya kiwanja katika aeneo lake kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Ibada,” alisema Chubugu.

Katika Ibada hiyo Askofu Malasusa alimtambulisha Gurtu na mkewe na kuwashukuru kwa moyo wao wa kutoa eneo hilo ambalo leo ni Usharika wa Kivule.

Chubungu alieleza kuwa baada ya kupata eneo hilo Washarika walikusanya nguvu wakaongeza eneo na hadi sasa neno la Usharika huo lina ukubwa mita za mraba 5,038 kisha wakajenga jengo la kuabudu la muda. Kabla ya kuwa na Mchungaji Mtaa Mtaa huo uliongozwa na Mwinjilisti wa kwanza Simon Nuru ambaye alikuwa mwajiriwa wa DMP na Mwinjilisti Shadrack Furaha ambaye alikuwa wa kujitolea.

Baadaye uliongozwa na Mwinjilisti Christowelu Mande ambaye wakati kwa sasa ni Mchungaji. Wainjilisti wengine walioongoza Usharika huo mteule ni Mtauye Mgode, Jason Kaseza na Emmanuel Mgaya.

Wachungaji walioongoza ni Nahori Chuma, Prosper Kinyaha na sasa Mch. Chuma. Usharika wa Kivule ambao sasa una Washarika 600 unatunza Mitaa ya Magole A na Msongola.

"Tumekuwa Usharika kwa hiyo hata majukumu yameongezeka kwa hiyo Washarika tunatakiwa kuwa na umoja ikibidi tuzidishe ili Usharika wetu uwe wa mfano, tunatakiwa kufuata taratibu na maagizo yote ya Dayosisi"