Wakati wakristo wakiwa wameanza Juma Takatifu, ambalo ni adhimisho la kukumbuka mateso, kifo na kufufuka kwa Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, wito umetolewa kwa wakristo kutoadhimisha juma hili kuu kwa mazoea, bali watambue thamani ya kazi aliyoifanya Yesu kwa ajili ya wokovu wao.

Akizungumza na Upendo Tv jijini Dar es Salaam, Askofu Mteule wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Mbilu amesema badala ya kuadhimisha kwa mazoea, wanatakiwa kutazama upya maisha yao, ili njia zao ziendane na mapenzi ya Mungu.