WAZAZI wametakiwa kuwapenda na kuwalea watoto katika maadili mema na yenye kumpendeza Mungu huku wakitambua huo ni mpango wa Mungu.

HAYO yalisemwa na Mchungaji Kiongozi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa pongwe Nkaleka Chedi wakati wa Ibada ya Sikukuu ya Mikaeli na Watoto iliyofanyika Usharikani hapo hivi karibuni.

Mch. Chedi alisema kuwa watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa ajili ya makusudi maalumu aliyoyaweka.

“Haijalishi mtoto amezaliwa ndani ya ndoa ama nje ya ndoa, mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu na Mungu anamleta duniani kwa makusudi maalum,” alisema.

“Watoto mnaowaona leo, ndiyo viongozi wa Kanisa kesho, miongoni mwao watakuwa Maaskofu, Wakuu wa majimbo, Wachungaji, Wainjilisti na Maparishiweka, wengine watakuwa walimu, madaktari, wabunge, mawaziri na hata Marais, kwa sasa huwezi kuona lakini Mungu amewandalia kusudi katika maisha yao alisema,” alisema.

Aliwaambiawazazi kuwa walipokuwa watoto walilelewa na wazazi wao ndiyo sababu wamekuwa jinsi walivyo kwa sababu ya wazazi wao kwa hiyo hata wao wakiwalea vizuri watoto wao watakuwa na thamani katika dunia hii.

Akifafanua juu Malaika Mikaeli, Mch. Chedi alisema kuwa Malaika huyo ni mlinzi na na kwamba watoto wanwekewa ulinzi wa Mungu kupitia malaika Mikaeli. Aliwataka wazazi kusimama imara kwenye malezi ya watoto wao na kueleza kuwa mtoto anapoangukia katika makundi mabaya kama ulevi, uvutaji sigara au wizi anayelaumika ni mzazi kwa sababu hakuweza kumlea na kumfunza malezi bora.

Picha ya mtandaoni/Fairplanet