JIMBO la Kaskazini la Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limefanikiwa kufikia vituo 12 ya kimisioni katika jimbo hilo na kuimarisha huduma za Kiinjili na kijamii wakati wa maadhimisho ya Juma la Misioni yaliyofikia kilele chake mwishoni mwa wiki iliyopita.

AKIZUNGUMZA na Upendo Media wakati akifunga Juma hilo katika Mtaa wa Kidomole, Mkuu wa Jimbo hilo Mchungaji Jacob Mwangomola alisema kuwa, watu mbalimbali wamempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao, huku wengine wakijiunga KKKT kutoka madhehebu mengine. Alivitaja vituo hivyo ambavyo ni Mitaa ya KKKT ni Msinune, Masuguru , Mambohela , Kiwangwa, Magogoni na Mkenge. Vingine ni Kidomole, Fukayose Shamba, Makulunge, Bomumaji

"Misioni ya mwaka huu imekuwa ya baraka sana, Mungu ametuhudumia sana,” alisema Mch. Mwangomola na kuongeza kuwa kazi kuu walizozifanya zilikuwa ni Uinjilishaji..."