PARISHIWEKA wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Usharika wa Kikarara, Agatha Eugene amesema kuwa njia pekee ya Mkristo kuvuna matunda mema ni kujenga uhusiano mzuri na Mungu pamoja na kutembea katika imani.

PARISHIWEKA Agatha aliyasema hayo wakati akifundisha ujumbe Neno la Mungu Usharikani hapo Jumapili iliyopita.

“Mungu anatamani awe karibu yetu siku zote kwa kutuongoza na kutuimarisha, hata kama mambo yameharibika anatamani atuchukue atuweke mahali sahihi kwa sababu ndani ya uwepo wake tunapata furaha na amani,” alisema.

Mtumishi huyo alisisitiza kwa kuwataka watu wenye nia ya kupata nguvu za Mungu kuwa na imani imara ili kuhakikisha wanaishi maisha ya kumpenda Mungu wakati wote.

Pia aliwahimiza watu wote kuutafuta uso wa Mungu kwa maombi na kwamba kwa kufanya hivyo wataijua kweli pamoja na kuepuka mafundisho potofu. Mtumishi huyo wa Mungu alihitimisha kwa kuwataka watu wote wenye uhitaji wa kupokea kibali kutoka kwa Mungu na kuhakikisha wanakuwa watu wenye niya ya kujifunza Neno.