MWINJILISTI wa KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Mbezi Beach, Stella Mhombo amewataka Wakristo kutozuiwa na vyeo na nafasi zao kukutana na Yesu. Akihubiri katika Ibada Jumapili iliyopita Usharikani hapo alieleza kuwa, mazingira, vyeo na vitu vingine vya dunia hii vitapita lakini Neno la Mungu litadumu milele.

“Ukitaka kukutana na Yesu asiyaangalie mazingira yako, usiangalie watu watasema nini, kuna watu wanataka kukutana na Mungu ila wanaangalia nafasi zao, vyeo vyao, nakuambia cheo kitapita lakini neno la Mungu halitapita,” alisema.

Pia aliwataka Washarika kujifunza kuwekeza kwa Mungu kwa sababu kuna faida nyingi za mwilini na rohoni. Aliwataka Wakristo kutoishi maisha ya kuwanyooshea vidole wengine na kuwahukumu kama wakosaji, wasiostahili kusamehewa.

Aidha aliwakumbusha kutoyakumbuka mambo ya zamani, kwani yanaweza kuwarudisha kwenye huzuni na kuwarudi nyuma kiimani.

SOMO

UKITAKA kukutana na Yesu asiyaangalie mazingira yako, usiangalie watu watasema nini, kuna watu wanataka kukutana na Mungu ila wanaangalia nafasi zao, vyeo vyao..