Wapendwa katika Kristo Yesu,

Siku hizi kila asubuhi huleta habari mpya zinazotushtusha, kutupa wasisi na hofu kuhusu ugonjwa unaoenea.

Neno langu kwa hali inayoendelea ni watu kutotaharuki na kuondoa hofu. Tunahitaji kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wataalam wa afya ikiwa ni pamoja kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kudumisha usafi wa mikono.

Uongozi wa Dayosisi umetoa maelekezo na tutaendelea kupeana taarifa na maelekezo kulingana na maendeleo ya ugonjwa huo.

Pia nawakumbusha wachungaji na washarika kuwa tayari kwa mabadiliko yoyote katika namna ya kumwabudu Mungu katika wakati huu

Tuendelee kumwomba na kuamini atatupitisha katika kipindi hiki.

“Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na upendo na ya moyo wa kiasi.“ (2. Tim. 1.7)

A.G.M.