Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa kwa umma na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) Machi 17, 2021 saa 5 usiku imeeleza kuwa Rais Magufuli amefariki dunia kwa maradhi ya Moyo akiwa katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli alilazwa tarehe 6 Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo wa mfumo wa umeme.

Nchi itakuwa katika kipindi cha maombolezo kwa siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti

#RIPMagufuli #RIPJPM