Wanawake wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, watatumia siku ya Ibada ya Tembea na Kristo kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Ibada hiyo itakayofanyika Aprili 5 mwaka huu katika Usharika wa Mbezi Luis, Dar es Salaam, itaongozwa na Msaidizi wa Askofu Dean Chediel Lwiza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Dayosisi, Dkt. Emmanuel Luvanda kila Usharika unatakiwa kuwa na wawakilishi wa wanawake 10.

“Kwa mwaka huu Ibada hii itaambatana na kuliombea Taifa la Tanzania amani, utulivu na faraja kutokana na msiba wa Kitaifa uliotupata pamoja na kumwombea Rais aliyepokea madaraka ili Mungu ampe hekima ya kuweza kuliongoza Taifa letu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.