Waumini wa KKKT wamekumbushwa kumtolea Mungu kwa moyo ili kuweka alama kwa lengo la kuendeleza Injili hususani katika maeneo ya misioni.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jimbo la Kusini Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mch Andrew King’omela wakati alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa juma la Misioni iliyofanyika katika viwanja vya Nyamisati wilayani Rufiji. 

“Unaposikia sadaka ya juma la misioni kubeba Usharika maana yake unawezesha Injili kufika katika maeneo ambayo ambayo hayajafikiwa,” alisema Mch. King’omela.

Mratibu wa Misioni wa jimbo hilo Mch. Edson Mgeni eneo hilo halina Kanisa la KKKT. Naye Mwinjilisti kutoka KKKT, Dayosisi ya Morogoro Eliakim Mwinuka aliwasihi Wakristo kumrudia Mungu ili kuurithi ufalme wa mbinguni.

Alisema kuwa bila kumtegemea Mungu, mwanadamu hatoweza kitu chochote, hivyo ni lazima akubali kuacha yote na kumkabidhi Mungu masiha yake ndipo Mungu atamwongoza katika njia yake na hatimaye ataweza kuurithi ufalme wa mbinguni.

Hivyo Juma la misioni huadhimishwa kila Jumapili ya mwisho wa mwezi Agosti kila mwaka, ikiwa ni ishara ya urithi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani kwa lengo la kumtangaza Kristo na kuadhimisha kuingia kwa injili katika Dayosisi hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 1887