WAZAZI na walezi wamehimizwa kuhakikisha wanawalea watoto katika misingi bora pasipo ubaguzi ili wawe viongozi bora watakao tumika ndani ya Kanisa na Taifa.

Wito huo umetolewe Jumapili iliyopita na Mkuu wa Jimbo la Arusha Mashariki, Dayosisi ya Kaskazini Kati, Mchg. Daniel Mahawe, wakatia kihubi ri katika Usharika Mteule wa IlMeshoroori Arusha, katika Ibada iliyoambatana na kuwaingiza kaziniviongozi wa Idara mbalimbali za Usharika huo Mteule.

“Mungu akikupa neema akakubariki, akakupa watoto hakikisha unawajali, unawaangalia na kutenda sawasawa, huwezi kujua nani watakao kuangalia baadaye,” alisema Mchg. Mahawe.

Mchg. Mahawe alilisisitiza kwa kusema kuwa, Wakristo wanapaswa kudumisha umoja na upendo ndani ya kanisa ili wawe mabalozi wazuri wakuwafanya wengine kumjua Mungu na kutambua kuwa umoja ni jambo la muhimu kwa maisha ya Mkristo.

“Ndugu zangu umoja wa Kanisa hili, umoja wa Usharika huu ndio nguvu ya Usharika huu, leo tunakumbuka habari za Kanisa letu KKKT, kutimiza miaka 59, tumeendelea kusimama hivi sababu ya umoja wetu, katika kulihubiri Neno la Mungu na katika kuyatunza mapokea mazuri ya Kanisa letu,” alisema.