Wakristo nchini wameungana na wakristo wengine Duniani Kote kusherekea sikukuu ya Pasaka ambayo ni kumbukumbu ya kufufuka kwa yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulubiwa, kufa na kuzikwa kwake.

Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. ALEX MALASUSA akihubiri leo katika ibada iliyofanyika katika Kanisa kuu la Azania Front amesema kuwa anatamani habari hizi za kufufuka kwa Yesu Kristo zipelekwe na kuzungumzwa katika maeneo ambayo yanahitaji kumjua Mungu

Amesema Yesu ana uwezo wa kubadili huzuni na kuleta furaha miongoni mwa watu waliokata tamaa, wanandoa na familia hivyo sikukuu hii ambayo ni kwa wakristo imfundishe kila mmoja kutambua kuwa uwezo wa Mungu hakuna mtu yoyote wa kuuzuwia na umeonekana katika kumfufua Yesu.

Askofu Dkt. MALASUSA amesema kuwa Yesu anatamani kuona watu wanaacha dhambi na kuutafuta utakatifu huku wakishudia habari zake kwa watu wengine wasiozijua na kuongeza kuwa wale walio katika dhambi wajihesabie kuwa wamekufa.