Karibu uhabarike kwa kusoma taarifa mbalimbali za Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront zilizojili katika kipindi cha kati ya mwezi Januari na Machi 2020. Miongoni mwa taarifa zilizopewa kipaumbele ni pamoja na;

  • Usharika waweka mipango madhubuti kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona
  • Mchungaji Chuwa awaaga washarika wa Azaniafront akihamia Mbezi Beach
  • Ibada ya Kiingereza yaanza kufanyika ndani ya jengo la Kanisa Kuu Azaniafront
  • Faragha ya Wazee wa Baraza yafanyika Bagamoyo
  • Azaniafront yaadhimisha siku ya wanawake duniani
  • Wanawake Azaniafront washiriki maombi ya dunia
  • Kwaya ya Agape yazuru Hospitali ya Taifa Muhimbili, yatoa misaada