Kusoma Biblia kwa kufuata mfumo wa kudukiza hufuata ngazi tatu tutakazoeleza hapa hatua kwa hatua. Hata hivyo  zinaweza kutokea wakati moja. Ngazi hizi tatu ni uchunguzi, ufafanuzi na matumizi.

Uchunguzi hujibu swali: fungu la Biblia linasema nini?  Huu ni msingi tunaohitaji kuweka tukitaka kufafanua na kutumia Neneo la Mungu. Je umashawahi kusoma aya, mlango au kitabu cha Biblia na dakika tano ulishindwa kukumbuka chochote ullichosoma? Mara nyingi tunasoma Biblia kwa macho yetu tu lakini bila kutumia akili yetu.

........................