Ofisi ya Mkaguzi wa Mali na Hesabu wa Dayosisi itakuwa na jukumu la kuhakikisha katiba , kanuni na miongozo ya dayosisi inafuatwa na kuzingatiwa katika ngazi zote za dayosisi. aidha itahakikisha kunakuwa na udhibiti wenye ufanisi wa rasilimali za dayosisi.

MALENGO NA WAJIBU WA OFISI

  • Kuhakikisha kuwa fedha zozote zinazotakiwa kutolewa kutoka akaunti za dayosisi matumizi yake yamepitishwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kwa mujibu wa kanuni;
  • Kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi yake yameidhinishwa zinatumika kwa kusudi lililokusudiwa na mamlaka iliyopitisha fedha hizo;
  • Kupitia mifumo ya udhibiti wa ndani mara kwa mara na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuiboresha;
  • Kufuatilia kwa karibu mabadiliko na maendeleo yote kuhusu ufuasi wa kanuni ya fedha na udhibiti wa ndani;
  • Kuandaa rasimu ya mipango (audit plan) ya utaratibu wa kuendesha kwa ufanisi kazi za ukaguzi katika dayosisi;
  • Kuandaa ripoti za tathimini ya viashiria vya hatari vinavyofungamana na utendaji;
  • Kuchunguza kwa makini mifumo na taratibu za uhasibu na kushauri namna ya kuiboresha.

Ofisi yetu

Emmanuel Msangi      Mkaguzi wa Mali na Hesabu ya Dayosisi     emma841@hotmail.com     +255 784 421 477

Elibariki Marco              Mkaguzi Mwandamizi                                       nasolwa1995@gmail.com   +255 679 622 711

Japhet Lukindo            Mkaguzi Mwandamizi                                       japhetjoseph@gmail.com     +255 712 251 021

Elizabeth Mollel            Mkaguzi                                                              elizamollel@yahoo.com         +255 762 782 362

Mary Mhalafu                Mkaguzi                                                              mhalafumary@gmail.com      +255 764 156 414